1Pigeni tarumbeta huko Siyoni;
pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu!
Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda,
maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,
naam, siku hiyo iko karibu!
2Hiyo ni siku ya giza na huzuni;
siku ya mawingu na giza nene.
Jeshi kubwa la nzige linakaribia
kama giza linalotanda milimani.
Namna hiyo haijapata kuweko kamwe
wala haitaonekana tena
katika vizazi vyote vijavyo.
3Kama vile moto uteketezavyo
jeshi hilo laharibu kila kitu mbele yake
na kuacha nyuma kila kitu kinateketezwa;
kabla hawajapita, nchi ni kama bustani ya Edeni,
lakini wakisha pita, ni jangwa tupu.
Hakuna kiwezacho kuwaepa!
4
amewapeni mvua ya kutosha:
Mvua za masika na mvua za vuli kama hapo awali.
24Mahali pa kupuria patajaa nafaka,
mashinikizo yatafurika divai na mafuta.
25Nitawarudishia miaka ile iliyoliwa na nzige,
kila kitu kilicholiwa na tunutu, parare na matumatu,
hilo jeshi kubwa nililowaletea!
26Mtapata chakula kingi na kutosheka;
mtalisifu jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,
aliyewatendea mambo ya ajabu.
Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
27Mtatambua kwamba mimi nimo miongoni mwenu,
enyi Waisraeli;
kwamba mimi Mwenyezi-Mungu,
ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine.
Watu wangu, kamwe hawatadharauliwa tena.
Siku ya Mwenyezi-Mungu28 “Kisha hapo baadaye
nitaimimina roho yangu juu ya binadamu wote.
Watoto wenu wa kike na wa kiume watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono.
29Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike,
nitaimimina roho yangu wakati huo.
30“Nitatoa ishara mbinguni na duniani;
kutakuwa na damu, moto na minara ya moshi.
31 Taz Mat 24:29; Marko 13:24-25; Luka 21:25; Ufu 6:12-13 Jua litatiwa giza,
na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,
kabla ya kufika siku ya Mwenyezi-Mungu,
siku iliyo kuu na ya kutisha.
32 Taz Rom 10:13 Hapo watu wote watakaoomba kwa jina la Mwenyezi-Mungu wataokolewa.
Maana katika mlima Siyoni na Yerusalemu,
watakuwako watu watakaosalimika,
kama nilivyosema mimi Mwenyezi-Mungu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.