Zaburi 82 - Swahili Common Language DC Bible

Mungu mtawala mkuu(Zaburi ya Asafu)

1Mungu anasimamia baraza lake;

anatoa hukumu katika kusanyiko la miungu:

2“Mpaka lini mtaendelea kuhukumu bila haki

na kuwapendelea watu waovu?

3Wapeni wanyonge na yatima haki zao;

tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara.

4Waokoeni wanyonge na maskini,

waokoeni makuchani mwa wadhalimu.

5“Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu!

Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu!

Misingi yote ya haki duniani imetikiswa!

6Mimi nilisema kuwa nyinyi ni miungu;

kwamba nyote ni watoto wa Mungu Mkuu!

7Hata hivyo, mtakufa kama watu wote;

mtaanguka kama mkuu yeyote.”

8Inuka ee Mungu, uuhukumu ulimwengu;

maana mataifa yote ni mali yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help