1Ee Mungu, usikie kilio changu,
usikilize sala yangu.
2Ninakulilia kutoka miisho ya dunia,
nikiwa nimevunjika moyo.
Uniongoze juu kwenye mwamba mkubwa
3maana wewe ndiwe kimbilio langu,
kinga yangu imara dhidi ya adui.
4Naomba nikae nyumbani mwako milele
nipate usalama chini ya mabawa yako.
5Ee Mungu, umezisikia ahadi zangu,
umenijalia sehemu yangu unayowapa wale wakuchao.
6Umjalie mfalme maisha marefu,
miaka yake iwe ya vizazi vingi.
7Atawale milele mbele yako, ee Mungu;
fadhili na uaminifu wako vimlinde.
8Hivyo nitakuimbia nyimbo za sifa,
nikizitekeleza ahadi zangu kila siku.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.