Zaburi 24 - Swahili Common Language DC Bible

Mfalme Mkuu(Zaburi ya Daudi)

1 Taz 1 Kor 10:26 Dunia na vyote vilivyomo ni vyake Mwenyezi-Mungu;

ulimwengu na wote waishio humo ni mali yake.

2Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari;

aliisimika imara juu ya mito ya maji.

3Nani atakayepanda mlima wa Mwenyezi-Mungu?

Nani atakayekaa katika hekalu lake takatifu?

4 Taz Mat 5:8 Ni mtu wa matendo mema na moyo safi,

asiyeuelekeza moyo wake katika upuuzi,

wala kuapa kwa uongo.

5Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu,

na haki yake kwa Mungu mwokozi wake.

6Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye;

naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo.

7Fungukeni enyi milango;

fungukeni enyi milango ya kale,

ili Mfalme mtukufu aingie.

8Ni nani huyo Mfalme mtukufu?

Ni Mwenyezi-Mungu, mwenye nguvu na uwezo;

Mwenyezi-Mungu, mwenye uwezo vitani.

9Fungukeni enyi malango,

fungukeni enyi milango ya kale,

ili Mfalme mtukufu aingie.

10Ni nani huyo Mfalme mtukufu?

Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi,

yeye ndiye Mfalme mtukufu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help