Sira UTANGULIZI - Swahili Common Language DC Bible

UTANGULIZIKitabu cha Hekima ya Sira (chajulikana pia kama “Eklesiastiko”) hapo awali kilikuwa kimeandikwa kwa Kiebrania yapata mwaka 180 K.K. Kitabu hiki kilitafsiriwa kwa Kigiriki na mjukuu wake. Mwandishi anatia sahihi kitabu chake kwa jina (50:27) na kusema juu ya kazi yake (39:1-11). Tunaambiwa hivyo na huyo mwana mjukuu katika utangulizi wa kitabu hiki. Makala ya Kigiriki ndiyo iliyotumiwa kutoa tafsiri hii ya Kiswahili.Kitabu chenyewe ni kimojawapo cha vitabu vijulikanavyo kama vitabu vya hekima, nacho chajumuika na umoja wa vitabu hivyo vya Agano la Kale katika kuonesha umoja wa maandishi ya sheria, maandishi ya manabii na ya vitabu vingine; hili ni jambo linalosisitizwa katika kitabu hiki, pamoja na mafunzo kuhusu uzoefu na “kumcha Bwana.” Ingawa Sira hakina muundo dhahiri, kinafanana na kitabu cha Methali kwa namna nyingi. Kinasisitiza mafundisho yaliyo kawaida ya hekima: Usemi unaofaa, utajiri na umaskini, uaminifu, nidhamu, uchaguzi wa marafiki, dhambi na kifo, tuzo na hekima.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help