Hagai UTANGULIZI - Swahili, Common Language Bible

UTANGULIZITunavyoambiwa mwanzoni mwa kitabu hiki, Hagai alihubiri kuanzia mwaka wa pili wa utawala wa Dario mfalme wa Persia, yaani katika mwaka wa 520 K.K., karibu miaka 20 baada ya Wayahudi waliokuwa uhamishoni Babuloni kuruhusiwa na mfalme wa Persia kurudi makwao. Kundi la kwanza la Waisraeli lilirejea makwao kuanzia mwaka wa 538 K.K. Baada ya Wayahudi kurejea makwao, walianza shughuli za kujenga upya hekalu lililoharibiwa na Wababuloni katika mwaka wa 587. Lakini walikata tamaa; ndio maana nabii anawatia moyo waendelee. Anawatangazia kwamba, hekalu jipya litapendeza kuliko lile la kwanza (2:1-9) na kwamba ujenzi wake utamaliza hali ya unajisi na umaskini uliowapata watu wa Mungu (2:10-20).Hagai aliwatia watu moyo kwa maneno yake, yaliyowahimiza watu wa nyakati zake wawe na bidii na kufanya kazi wakitazamia hali mpya ambayo Mungu amewatayarishia.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help