Zaburi 67 - Swahili, Common Language Bible

Wimbo wa shukrani(Kwa Mwimbishaji: Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo)

1Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki;

utuelekezee uso wako kwa wema;

2dunia yote ipate kutambua njia yako,

mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa.

3Watu wote wakutukuze, ee Mungu;

watu wote na wakusifu!

4Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha;

maana wawahukumu watu kwa haki,

na kuyaongoza mataifa duniani.

5Watu wote wakutukuze, ee Mungu;

watu wote na wakusifu!

6Nchi imetoa mazao yake;

Mungu, Mungu wetu, ametubariki.

7Mungu aendelee kutubariki.

Watu wote duniani na wamche.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help