1Kura ya pili ilizipata koo za kabila la Simeoni na sehemu yao ya nchi ilikuwa imezungukwa na ile ya kabila la Yuda.
2Kabila la Simeoni lilipata miji ya Beer-sheba, Sheba, Molada
3Hasar-shuali, Bala, Esemu,
4Eltoladi, Bethuli, Horma,
5Siklagi, Beth-markabothi, Hasar-susa,
6Beth-lebaothi na Sharuheni. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake.
7Pia kulikuwa na miji ya En-rimoni, Etheri, na Ashani. Jumla ya miji waliyopewa ni minne pamoja na vijiji vyake.
8
35Miji yao iliyokuwa na ngome ni Zidimu, Zeri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,
36Adama, Rama, Hazori,
37Kedeshi, Edrei, En-hazori,
38Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake.
39Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Naftali; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Nchi ya kabila la Dani40Kura ya saba ilizipata koo za kabila la Dani.
41Eneo la nchi yao lilikuwa na miji ya Sora, Eshtaoli, Ir-shemeshi
42Shaalabini, Aiyaloni, Yithla,
43Eloni, Timna, Ekroni
44Elteke, Gibethoni, Baalathi,
45Yehudi, Bene-beraki, Gath-rimoni,
46Me-yarkoni na Rakoni na nchi iliyokuwa karibu na Yopa.
47Taz Amu 18:27-29 Watu wa kabila la Dani walipopoteza nchi yao, walikwenda na kuushambulia mji wa Leshemu. Waliushinda na kuuteka, na baada ya kuwaua wakazi wake wote, waliumiliki halafu wakabadili jina la mji huo kuwa Dani; jina ambalo lilikuwa ni la babu yao.
48Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Dani; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Ugawanyaji wa mwisho49Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.
50Kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu walimpa mji ambao aliuchagua yeye mwenyewe, yaani Timnath-sera, ambao ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Naye Yoshua akaujenga upya mji huo na kukaa humo.
51Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.