Zaburi 13 - Swahili, Common Language Bible

Kuomba msaada(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)

1Mpaka lini ee Mwenyezi-Mungu, utanisahau?

Je, utanisahau mpaka milele?

Mpaka lini utanificha uso wako?

2Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini,

na sikitiko moyoni siku hata siku?

Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu?

3Uniangalie na kunijibu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu.

Uyaangazie macho yangu, nisipatwe na usingizi wa kifo.

4Usiwaache maadui zangu waseme: “Tumemweza huyu!”

Watesi wangu wasije wakafurahia kuanguka kwangu.

5Lakini mimi nazitumainia fadhili zako;

moyo wangu na ufurahie wokovu wako.

6Nitakuimbia wewe, ee Mwenyezi-Mungu,

kwa ukarimu mwingi ulionitendea!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help