1Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:
2“Wewe mtu! Tega kitendawili, uwaambie fumbo Waisraeli.
3Waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:
Kulikuwa na tai mmoja mkubwa sana
aliyekuwa na mabawa makubwa,
yenye manyoya marefu mengi
yenye rangi za kila aina.
Tai huyo aliruka mpaka mlimani Lebanoni,
akatua juu ya kilele cha mwerezi;
4akakwanyua tawi lake la juu zaidi,
akalipeleka katika nchi ya wafanyabiashara,
akaliweka katika mji wao mmoja.
5Kisha akachukua mmea mchanga nchini Israeli,
akaupanda katika ardhi yenye rutuba
ambako kulikuwa na maji mengi.
6Mmea ukakua ukawa mzabibu
wa aina ya mti utambaao;
matawi yake yakamwelekea,
na mizizi yake ikatanda chini yake.
Mzabibu ukachipua matawi na majani mengi.
7Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa;
alikuwa na mabawa makubwa ya manyoya mengi.
Basi, ule mzabibu ukamtandia mizizi yake,
ukamwelekezea matawi yake,
ili aumwagilie maji.
8Mzabibu ulikuwa umetolewa kitaluni mwake
ukapandikizwa penye udongo mzuri na maji mengi,
ili upate kutoa matawi na kuzaa matunda
uweze kuwa mzabibu mzuri sana!
9Sasa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nakuuliza:
Je, mzabibu huo utaweza kustawi?
Je, hawatangoa mizizi yake
na kuozesha matunda yake
na matawi yake machanga kuyanyausha?
Hakutahitajika mtu mwenye nguvu au jeshi
kuungoa kutoka humo ardhini.
10Umepandikizwa, lakini, je, utastawi?
Upepo wa mashariki uvumapo juu yake utanyauka;
utanyauka papo hapo kwenye kuta ulikoota.”
Maelezo yake11Kisha neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
12
24Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.