Habakuki UTANGULIZI - Swahili, Common Language Bible

UTANGULIZIYaonekana kwamba Habakuki alifanya huduma yake ya kinabii katika Yuda yapata mwaka 600 K.K. Huo ulikuwa wakati wa utawala wa mfalme Yehoyakini. Wakati huo Wababuloni ndio taifa lililokuwa na nguvu huko Mashariki ya Kati na liliyakandamiza na kupora mali za mataifa mengine, mojawapo likiwa taifa la Yuda. Habakuki alipinga jambo hilo la uonevu wa wadogo na taifa baya lenye dhambi. Aliuliza katika 1:13: “Kwa nini (Mungu) unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao?” Jibu la Mungu ni kwamba yeye atafanya kitu kwa wakati wake na hadi wakati huo: Wenye kiburiwataangamia; lakini waadilifu wataishi kwa kumwamini Mungu (2:4).Sehemu ya mwisho ya kitabu hiki ni sala, na katika sala hiyo nabii anaeleza ukuu wake Mungu, kisha anasisitiza juu ya imani kwa Mungu.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help