Isaya 66 - Swahili, Common Language Bible

Ibada ya uongo na ya kweli

1

2Mimi mwenyewe nilivifanya vitu hivi vyote,

na hivi vyote ni mali yangu.

Lakini ninachojali mimi

ni mtu mnyenyekevu na mwenye majuto,

mtu anayetetemeka asikiapo neno langu.

3“Lakini watu hawa wanafanya wanavyotaka:

Wananitolea tambiko ya ng'ombe

na mara wanaua watu kutambikia.

Wananitolea sadaka ya mwanakondoo

na pia wanamvunja mbwa shingo.

Wananitolea tambiko ya nafaka

na pia kupeleka damu ya nguruwe.

Wanachoma ubani mbele yangu

na kwenda kuabudu miungu ya uongo.

Hao wamechagua kufuata njia zao wenyewe.

4Basi, nitawaletea taabu;

yatawapata yaleyale wanayoyahofia;

maana nilipoita hakuna aliyeitika,

niliponena hawakusikiliza.

Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu,

walichagua yale ambayo hayanipendezi.”

Adhabu na wokovu

5Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,

enyi msikiao neno lake mkatetemeka:

“Ndugu zenu ambao wanawachukia,

na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu,

wamesema kwa dharau

‘Mungu na aoneshe utukufu wake,

nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’

Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!

6Sikilizeni, ghasia kutoka mjini,

sauti kutoka hekaluni!

Hiyo ni sauti ya Mwenyezi-Mungu

akiwaadhibu maadui zake!

7 Ludi, nchi zenye wapiga upinde stadi; watakwenda pia Tubali na Yowani na nchi ambapo watu hawajapata kusikia umaarufu wangu wala kuuona utukufu wangu. Hao wajumbe wangu watautangaza utukufu wangu katika mataifa hayo.

20Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

21Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

22 66:22 Taz Isa 65:17; 2Pet 3:13; Ufu 21:1 “Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumba

zitakavyodumu milele kwa uwezo wangu,

ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.

23Katika kila sikukuu ya mwezi mpya,

na katika kila siku ya Sabato,

binadamu wote watakuja kuniabudu.

Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

24 66:24 Taz Marko 9:48 “Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help