Zaburi 126 - Swahili, Common Language Bible

Kuomba nguvu mpya(Wimbo wa Kwenda Juu)

1Mwenyezi-Mungu alipoturekebisha na kuturudisha Siyoni,

tulikuwa kama watu wanaoota ndoto!

2Hapo tuliangua kicheko;

tulishangilia kwa furaha.

Nao watu wa mataifa mengine walisema:

“Mwenyezi-Mungu amewatendea mambo makubwa!”

3Kweli Mwenyezi-Mungu alitutendea mambo makubwa,

tulifurahi kwelikweli!

4Ee Mwenyezi-Mungu, urekebishe tena hali yetu,

kama mvua inavyotiririsha maji katika mabonde makavu.

5Wanaopanda kwa machozi,

watavuna kwa shangwe.

6Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia,

watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help