Waebrania 10 - New Testament: Easy-to-Read Translation

Yesu Kristo, Dhabihu Pekee Tunayoihitaji

1Sheria ya Musa ilitupa sisi picha tu isiyo wazi sana ya mambo yaliyokuwa yanakuja baadaye. Sheria siyo picha kamili ya mambo halisi. Sheria huwaambia watu kutoa sadaka zile zile kila mwaka. Wale wanaokuja kumwabudu Mungu wanaendelea kutoa sadaka. Lakini sheria haiwezi kamwe kuwakamilisha wao.

2Kama sheria ingeweza kuwakamilisha watu, sadaka hizi zingekuwa zimekoma. Tayari wao wangekuwa safi kutoka katika dhambi, na bado wasingehukumiwa moyoni mwao.

3Lakini hayo siyo yanayotokea. Dhabihu zao zinawafanya wazikumbuke dhambi zao kila mwaka,

4kwa sababu haiwezekani kwa damu ya fahali na mbuzi kuondoa dhambi.

5Hivyo baada ya Kristo kuja ulimwenguni alisema:

“Huhitaji sadaka na sadaka,

lakini umeandaa mwili kwa ajili yangu.

6Hukuridhishwa na sadaka za kuteketezwa

na sadaka kuondoa dhambi.

7Kisha nikasema, ‘Nipo hapa, Mungu.

Imeandikwa juu yangu katika kitabu cha sheria.

Nimekuja kufanya yale unayopenda.’”

8Kwanza Kristo alisema, “Wewe hufurahishwi na sadaka na sadaka. Hukuridhishwa na sadaka za kuteketezwa na sadaka ili kuondoa dhambi.” (Hizi ndizo sadaka zote ambavyo sheria inaagiza.)

9Kisha akasema, “Niko hapa, Mungu. Nimekuja kufanya yale unayopenda.” Hivyo Mungu akafikisha mwisho wa mfumo wa zamani wa utoaji sadaka na akaanzisha njia mpya.

10Yesu Kristo alifanya mambo ambayo Mungu alimtaka ayafanye. Na kwa sababu ya hilo, tunatakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Kristo. Kristo aliitoa sadaka hiyo mara moja, inayotosha kwa nyakati zote.

11Kila siku makuhani husimama na kutekeleza shughuli zao za kidini. Tena na tena hutoa sadaka zilezile, ambazo kamwe haziwezi kuondoa dhambi.

12Lakini Kristo alitoa sadaka moja tu kwa ajili ya dhambi, na sadaka hiyo ni nzuri kwa nyakati zote. Kisha akakaa mkono wa kuume wa Mungu.

13Na sasa Kristo anawasubiria hapo adui zake wawekwe chini ya mamlaka yake.

14Kwa sadaka moja Kristo akawakamilisha watu wake milele. Ndio wale wanaotakaswa.

15Roho Mtakatifu pia anatuambia juu ya hili. Kwanza anasema:

16“Hili ndilo agano nitakaloweka

na watu wangu baadaye, asema Bwana.

Nitaziweka sheria zangu ndani ya mioyo yao.

Nitaziandika sheria zangu katika fahamu zao.”

17Kisha anasema,

“Nitazisahau dhambi zao

na nisikumbuke kamwe uovu walioutenda.”

18Na baada ya kila kitu kusamehewa, hakuna tena haja ya sadaka ili kuziondoa dhambi.

Mkaribieni Mungu

19Hivyo ndugu na dada, tuko huru kabisa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu. Tunaweza kufanya hivi bila hofu kwa sababu ya sadaka ya damu ya Yesu.

20Tunaingia kwa njia mpya ambayo Yesu alitufungulia. Ni njia iliyo hai inayotuelekeza kupitia pazia; yaani mwili wa Yesu.

21Na tunaye kuhani mkuu zaidi anayeisimamia nyumba ya Mungu.

22Ikiwa imenyunyiziwa kwa damu ya Kristo, mioyo yetu imewekwa huru kutokana na dhamiri yenye hukumu, na miili yetu imeoshwa kwa maji safi. Hivyo mkaribieni Mungu kwa moyo safi, mkijaa ujasiri kwa sababu ya imani katika Kristo.

23Tunapaswa kuling'ang'ania tumaini tulilonalo, bila kusitasita kuwaeleza watu juu yake. Tunaweza kumwamini Mungu kuwa atatimiza aliyoahidi.

Saidianeni Ninyi kwa Ninyi Kuwa Imara

24Tunahitaji kumfikiria kila mtu kuona jinsi tunavyoweza kuhamasishana kuonesha upendo na kazi njema.

25Tusiache kukutana pamoja, kama wanavyofanya wengine. Hapana, tunahitaji kuendelea kuhimizana wenyewe. Hili linazidi kuwa muhimu zaidi na zaidi kadri mnavyoona ile Siku inakaribia.

Msigeuke Mbali ya Mwana wa Mungu

26Kama tutaamua kuendelea kutenda dhambi baada ya kujifunza ukweli, ndipo hakutakuwa sadaka nyingine itakayoondoa dhambi.

27Tukiendelea kutenda dhambi, kitakachokuwa kimebaki kwetu ni wakati wa kutisha wa kuingoja hukumu na moto wa hasira utakaowaangamiza wale wanaoishi kinyume na Mungu.

28Yeyote aliyekataa kuitii Sheria ya Musa alipatikana ana hatia kutokana na ushuhuda uliotolewa na mashahidi wawili au watatu. Watu wa jinsi hiyo hawakusamehewa. Waliuawa.

29Hivyo fikiri jinsi watu watakavyostahili kuhukumiwa zaidi ambao wanaonesha kumchukia mwana wa Mungu; watu wanaoonesha kuwa hawana heshima kwa sadaka ya damu iliyoanzisha agano jipya na mara moja ikawatakasa au wale wanaomkashifu Roho wa neema ya Mungu.

30Tunajua kuwa Mungu alisema, “Nitawaadhibu watu kwa ajili ya makosa wanayofanya”;

39Lakini sisi siyo wale wanaogeuka nyuma na kuangamia. Hapana, sisi ni watu walio na imani na tunaokolewa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help