1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda kwenye kilima na kukaa chini. Wanafunzi wake walimjia Yesu.
2Kisha Yesu akaanza kuwafundisha watu kwa akasema:
3“Heri kwa walio maskini na wenye kujua kwamba wanamhitaji Mungu.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
4Heri kwa wenye huzuni sasa.
Kwa kuwa watafarijiwa na Mungu.
5Heri kwa walio wapole.
Kwa kuwa watairithi nchi.
6Heri kwa wenye kiu na njaa ya kutenda haki.
Kwa kuwa Mungu ataikidhi kiu na njaa yao.
7Heri kwa wanaowahurumia wengine.
Kwa kuwa watahurumiwa pia.
8Heri kwa wenye moyo safi,
Kwa kuwa watamwona Mungu.
9Heri kwa wanaotafuta amani.
Kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.
10Heri kwa wanaoteswa kwa sababu ya kutenda haki.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
11Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi.
12Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.
Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)13Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yoyote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14Ninyi ni nuru inayong'aa ili ulimwengu uweze kuiona. Ni kama mji uliojengwa juu ya kilima unavyoonekana wazi.
15Watu hawawashi taa na kuificha kwenye chungu. Bali huiweka kwenye kinara cha taa ili nuru iangaze kwa kila mtu.
16Kwa namna hiyo hiyo mnapaswa kuwa nuru kwa ajili ya watu wengine. Hivyo ishini katika namna ambayo watakapoyaona matendo yenu mema, watamtukuza Baba yenu wa mbinguni.
Yesu Afundisha Kuhusu Sheria ya Musa17Msifikiri kwamba nimekuja kuiharibu Sheria ya Musa au mafundisho ya manabii. Sikuja kuyaharibu mafundisho yao bali kuyakamilisha.
18Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.
19Kila mtu anapaswa kutii kila amri iliyo katika sheria, hata ile isiyoonekana kuwa ya muhimu. Kila atakayevunja mojawapo ya amri hizi ndogo na kuwafundisha wengine kuzivunja atahesabiwa kuwa ni mdogo sana katika ufalme wa Mungu. Lakini kila anayeitii na kuwafundisha wengine kuitii sheria atakuwa mkuu katika ufalme wa Mungu.
20Ninawambia, ni lazima muitii sheria ya Mungu kwa kiwango bora kuliko kile cha walimu wa sheria na Mafarisayo. La sivyo, hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
Yesu Afundisha Kuhusu Hasira21Mmesikia kuwa hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Usimwue yeyote. Na yeyote atakayeua atahukumiwa.’ nenda maili mbili pamoja naye.
42Mpe kila anayekuomba, usimkatalie anayetaka kuazima kitu kwako.
Wapende Adui Zako(Lk 6:27-28,32-36)43Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Wapende rafiki zako alionao baba yenu wa Mbinguni kwa watu wote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.