Warumi 10 - New Testament: Easy-to-Read Translation

1Kaka na dada zangu, ninalotamani zaidi ni kwamba Waisraeli wote waokolewe. Hayo ndiyo maombi yangu kwa Mungu.

2Naweza kusema hili juu yao: Kwa hakika wana bidii sana ya kumtii Mungu, lakini hawaijui njia iliyo sahihi.

3Hawakuelewa kile ambacho Mungu alifanya ili kuwaokoa watu. Hivyo walijaribu kwa njia yao wenyewe kupata kibali kwa Mungu kwa kuishika sheria. Na wakakataa kuifuata njia ya Mungu ya kuwaokoa watu.

4Sheria ilifikia mwisho wake wakati Kristo alipolikamilisha kusudi lake. Sasa kila mtu anayeiweka imani yake kwake anahesabiwa haki mbele za Mungu.

5Musa anaandika juu ya kuhesabiwa haki kwa kuifuata sheria. Anasema: “Ili kupata uzima katika sheria imempasa mtu kuzitii.” ili kupata msaada, ataokolewa.”

14Lakini watu watawezaje kumwita Bwana na kupata msaada wake ikiwa hawamwamini yeye? Na watawezaje kumwamini Bwana ikiwa hawajawahi kuzisikia habari zake? Na watawezaje kuzisikia habari zake ikiwa hayupo mtu wa kuwaambia?

15Na mtu atawezaje kwenda na kuwaambia habari hizo ikiwa hajatumwa? Haya, hii ndiyo sababu Maandiko yanasema, “Ni jambo la kufurahisha kumwona mtu anayepeleka Habari Njema!”

16Lakini si watu wote walizipokea Habari Njema hizo. Na hii ndiyo sababu Isaya alisema, “Bwana, nani aliyeamini yale tuliyowaeleza?”

19Lakini tena nauliza, “Je! watu wa Israeli hawakuelewa?” Ndiyo, walielewa. Musa alikuwa wa kwanza kujibu swali hili. Na anasema haya kwa ajili ya Mungu:

“Nitawatumia wale ambao siyo Taifa halisi ili liwafanye muone wivu.

Nitalitumia taifa ambalo halielewi ili mkasirike.”

20Kisha Isaya ana ujasiri wa kutosha kusema haya kwa ajili ya Mungu:

“Watu walionipata mimi hawakuwa wakinitafuta.

Nilijitambulisha kwa watu ambao hawakuwa wakinitafuta.”

21Lakini kuhusu watu wa Israeli Mungu anasema,

“Kutwa nzima nilisimama nikiwa tayari kuwakubali watu hawa,

lakini ni wakaidi na wamekataa kunitii.”

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help