1Nazungumza nayi sasa kama mmojawapo niliye wa Kristo. Hivyo mnaweza kuwa na uhakika kuwa sisemi uongo. Dhamiri yangu, inayotawaliwa na Roho Mtakatifu, inakubali kwamba ninayowaambia sasa ni kweli.
2Nimejawa na huzuni na maumivu ya moyoni yasiyokwisha
3kwa ajili ya watu wangu. Wao ni kaka na dada zangu katika mwili. Natamani ningeweza kuwasaidia. Ningekuwa tayari pia kuomba kupokea laana ya kutengwa na Kristo kama hiyo itaweza kuwasaidia.
4Ni Waisraeli, watoto waliochaguliwa na Mungu. Wameushuhudia utukufu wa Mungu na wanashiriki maagano aliyofanya Mungu na watu wake. Mungu aliwapa Sheria ya Musa, ibada ya Hekalu, na ahadi zake.
5Ni wazaliwa wa mababa zetu wakuu, na ni familia ya kidunia ya Masihi, ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote. Yeye asifiwe milele! Amina.
6Sina maana kuwa Mungu alishindwa kutimiza ahadi yake kwa Wayahudi. Lakini kwa hakika ni baadhi tu ya Waisraeli ndiyo watu wa Mungu.
7Na hivyo ni baadhi tu ya watoto wa Abrahamu ndiyo wazaliwa wake halisi. Hivi ndivyo Mungu alimwambia Abrahamu: “Wazaliwa wako halisi watakuwa wale waliotoka kwa Isaka.”
10Na si hivyo tu. Kitu kama hicho kilimtokea Rebeka ambaye baada ya kupata mimba ya wana wawili mapacha waliotokana na baba mmoja, baba yetu Isaka.
11-12Ndiyo, kabla ya kuzaliwa wana hao mapacha, Mungu alimwambia Rebeka, “Mwana mkubwa atamtumikia mdogo.”
14Namsikia mtu akiuliza, “Hivyo hii ina maana gani? Je! Mungu si mwenye haki?” Hapana!
15Mungu alimwambia Musa, “Nitampa rehema yeyote ninayetaka kumpa rehema. Nitamhurumia yeyote ninayemchagua.”
26Na pale Mungu aliposema zamani:
‘Ninyi si watu wangu’;
hapo wataitwa watoto wa Mungu aliye hai.”
27Na Isaya huililia Israeli:
“Wako watu wengi sana wa Israeli,
kuliko mchanga ulio pwani ya baharini.
Lakini wachache wao watakaookolewa.
28Ndiyo, Bwana atakamilisha kwa haraka
aliyosema atayafanya duniani.”
29Ni kama vile alivyosema Isaya:
“Ikiwa Bwana Mwenye Uweza wote
asingewaruhusu watu wachache wakaishi,
tungekuwa tumeangamizwa kabisa,
kama vile miji miovu ya Sodoma, na Gomora.”
30Hivyo haya yote yanamaanisha nini? Je! tunasema kwamba watu wasio Wayahudi walifanikiwa kukipata kibali cha Mungu, hata kama hawakuwa wakijaribu kukipata kibali hicho? Ndiyo. Walipata kibali hicho kwa sababu ya imani kwa Mungu.
31Na vipi kuhusu watu wa Israeli? Wao walitaka kujipatia kibali cha Mungu kwa kuifuata sheria. Je! tunasema kuwa hawakufanikiwa?
32Ndiyo, na sababu yake ni hii: Walijitahidi kukipata kwa kufanya kwa usahihi mambo yote yaliyoamriwa katika sheria badala ya kumtumaini Mungu. Walijikwaa kwenye jiwe linalowafanya watu waanguke.
33Maandiko yanazungumza kuhusu jiwe hilo:
“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni litakalowafanya watu wajikwae.
Ni mwamba utakaowaangusha watu.
Lakini yeyote atakayemtumaini yeye
hataaibika kamwe.”
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.